Klabu ya Southampton inaripotiwa kuwa tayari kumuuza nyota wake anayewindwa na Chelsea, Graziano Pelle baada ya kukamilisha usajili wa staa mwingine, Charlie Austin.

Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, klabu hiyo ya Saints inaamini kwamba itakuwa na faida ya kumpa Pelle mkataba mpya kutokana na umri wake wa miaka 30 alionao.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu, Chelsea imekuwa ikihusishwa na mastraika kadhaa na kutokana na majeraha yanayomkabili kwa sasa nyota wao Diego Costa, inaweza ikashuhudiwa timu hiyo ikiongeza kasi ya kumfukuzia mchezaji huyo.

Arsenal Wachokonoa Jambo Chelsea FC
John Terry Ategemea Miujiza Stamford Bridge