Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imewasili salama mjini Cotonou-Benin tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kundi F wa kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2023, dhidi ya Niger.

Stars itacheza kesho Jumamosi (Juni 04) katika Uwanja wa taifa wa nchi hiyo (Stade de l’Amitie) ambao unatumiwa na timu ya taifa ya Niger kama uwanja wake wa nyumbani kufuatia Uwanja wa taifa wa nchi hiyo (Stade Seyni Kountché) kushindwa kufikia vigezo vya CAF.

Shirikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’ limethibitisha kuwasili salama kwa Taifa Stars kwa kuweka picha ya Video kwenye Mitandao yake ya Kijamii, ikionyesha wachezaji wakishuka kwenye Ndege Uwanja wa Ndege wa Benin.

Stars iliondoka jijini Dar es salaam jana Alhamis (Juni 02) majira ya jioni, huku wachezaji wakionekana kuwa na ari ya kupambana kwenye mchezo dhidi ya Niger.

Baada ya mchezo wa kesho Jumamosi (Juni 04), Stars itarejea jijini Dar es salaam kucheza mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Kundi F dhidi ya Algeria utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 08.

Fiston Mayele kutimka Young Africans
Ahmed Ally: Tutafanya usajili mkubwa msimu ujao