Tanzania imefanikiwa kuvunja rekodi ya Uganda kwa tamasha la JAMAFEST kuhudhuriwa na watu wengi zaidi toka lilipozinduliwa jumapili iliyopita na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linatarajiwa kuhitimishwa leo limefanikiwa kuvuka matarajio yaliyowekwa, akizungumza jana mkurugenzi msaidizi idara ya habari maelezo Rodney  Mbuya, amesema mwamko umekuwa mkubwa katika tamasha hilo na Tanzania imefanikiwa kuvunja rekodi ya Uganda ya mwaka 2017.

”Mara  nyingi nyakati za jioni watu wengi huwa kwenye tamasha wakishatoka makazini wanakuja kuburudika kwahiyo tumevunja rekodi tupo vizuri sana ”amesema  Mbuya

Mbuya amesema sababu za wasanii wa bongo fleva kupewa nafasi  ya kutumbuizwa katika tamasha hilo ikiwa ni moja ya mpango wa aina zote za sanaa zionekane.

Tamasha hilo liliopambwa na wasanii wa kizazi kipya lilikuwa na mvuto wa aina yake katika burudani kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, aliyefanikiwa kutumbuizwa katika uzinduzi wa tamasha hilo wikendi iliyopita, huku wengine ni Barnaba Classic, Mario, Dj D Ommy, Jux, G Nako, Mboso, Maua sama, Navy Kenzo, Country boy na wengine wengi.

Mwaka 2017 tamasha hilo lilifanyika nchini Uganda ambapo watu zaidi ya 46,000 walishuhudia tamasha la tatu la jumuiya ya Afrika  Mashariki  la utamaduni ‘JAMAFEST’.

 

 

 

DC Kilolo abadili madereva 10 kwa miaka minne
Majaliwa ashusha rungu kwa Watendaji kata, Ujauzito kwa wanafunzi