Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya uchimbaji madini ya Nickel, LZ Nickel Ltd kutoka  Uingereza ambapo faida itakuwa ni nusu kwa nusu baina ya mataifa hayo mawili.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini ambayo imefanyika Bukoba mkoani Kagera Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Madini kuhakikisha makubaliano kati yake na kampuni ya LZ Nickel Ltd yanatekelezwa kwa muda mfupi ili mradi wa uchimbaji wa madini wa Kabanga uanze kutekelezwa mapema.

Aidha, Rais Magufuli amesema endapo uchimbaji huo utaanza mapema, mwaka huu kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa ajira za watu milioni 8.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema mradi huo wa Kabanga uligunduliwa kutokana na utafiti uliofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia uhisani wa UNDP  kuanzia mwaka 1976-1979 ambao ulibainishwa uwepo wa Madini ya Nickel.

Waziri Kabudi ametaja faida za mradi huo kuwa ni pamoja na mapato mrabaha, kodi , gawio lakini pia amesema fedha zote zitakazotokana na mauzo ya madini hayo zitahifadhiwa katika akaunti za benki zilizopo Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini , David Concar amesema mradi wa uchimbaji wa madini ya Nickel unaotekelezwa na kampuni ya Uingereza umekuja muda muafaka na hautakuwa na madhara makubwa ya mazingira.

Watumishi sekta ya afya hatiani kwa ubadhirifu wa dawa
Danny Drinkwater atimkia Uturuki

Comments

comments