Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji SportPesa Tanzania Tarimba Abbas amesema, suala la Klabu ya Young Africans kusaini mkataba na Kampuni nyingine na kuipa haki wa kuweka Tangazo sehemu ya kifuni ya jezi zao, bado linaendelea kuwakera.

Young Africans iliingia Mkataba na Kampuni ya Hier mapema mwezi huu, kwa ajili ya kuidhamini Klabu hiyo katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi, kwa kuepuka udhamini wa Kampuni ya Kubashiri, ambao kikanuni hautakiwi kwenye hatua hiyo.

Akihojiwa na Clouds TV mapema leo Jumanne (Februari 28), Tarimba amesema hadi sasa hawajafurahishwa na kitendo cha Young Africans kusaini mkataba huo, lakini wlaichokifanya ni kutumia busara ili kulisaidia Soka la Tanzania kutimiza azma yake ya kusonga mbele.

Amesema wanaamini Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo Kongwe nchini Tanzania wanaona wapo sawa, lakini ukweli ni kwamba hawako sawa kimkataba na kisheria.

“Sisi kama Sportpesa suala la mkataba wetu na Klabu ya Young Africans hatujaridhika, nasisitiza hatujaridhika kwa sababu hatujafanyiwa sawa lakini wao Young Africans kwa upande wao wanaona wamefanya sawa.”

“Tukianza kubishana hatutausaidia Mpira wa Tanzania, Lengo letu ni kuusaidia mpira wa Tanzania.” amesema Tarimba

Siku moja baada ya Young Africans kusaini mkataba na Kampuni ya Hier, Kampuni ya SportPesa ilitoa taarifa ya kusikitishwa na kupinga mpango huo, hali ambayo ilizua taharuki kwa wadau wa soka la Bongo.

Harmonze aomba msaada madai ya pesa zake
Rais apokea Bil.16 za mahitaji ya dharula