Takriban watu sita wameokolewa wakiwa hai chini ya vifusi nchini Uturuki, huku idadi ya vifo ikifikia watu 21,000, kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo na ile ya Syria.
Watu hao, wameokolewa ikiwa yamepita zaidi ya masaa 101 baada ya kutokea tetemeko la ardhi ambalo limeacha simanzi na majonzi kwa familia nyingi.
Mmoja wa maafisa wa uokozi, Murat Baygul amesema manusura walikuwa walikutwa wakiwa wamekumbatiana katika sehemu iliyosalia kwenye upenyo wa jengo lililoporomoka.
Februari 6, 2023 tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lilikumba eneo la mpakani kati ya Uturuki na Syria, ambako kuna wakazi zaidi ya milioni 13.5.