Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana baada ya wanasheria wawili, Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu kumwekea dhamana hiyo.
Lissu alikamatwa ghafla alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, baada ya mashitaka yake ya uchochezi kufutwa katika kesi zinazomkabili.
Aidha, Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lissu alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini katika jamii wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani, Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.
Hata hivyo, baada ya mahojiano hayo, Lissu ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.

Arsenal Ya Arsene Wenger Kupindua Matokeo Leo?
Video: Aliyempa ardhi Makonda ahojiwa na Polisi, Lipumba awatumbua wakurugenzi 5 Z'bar