Ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya – EU nchini Nigeria, umekosoa ukosefu wa uwazi na utendaji usiordhisha wa INEC, wakati wa utoaji wa matokeo yake ya awali.

Waangalizi hao wamesema, wana imani juu ya uhuru na weledi wa Tume ya uchaguzi tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi huo lakini imani ya umma ilipungua kutokana na mipango mibovu na mawasiliano ya uhakika hapo awali na siku ya uchaguzi.

Ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya – EU. Picha ya Voice of Nigeria.

Aidha, wamesema walibaini kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa na taratibu za upigaji kura hazikufuatwa huku baadhi ya makosa ya tume yakiwafanya wapinzani kususia zoezi la kuhesabu kura kwa baadhi ya maeneo.

Hatua nyingine iliyokosolewa ni pamoja na upakiaji wa matokeo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kutofaulu, na hivyo kuzua wasiwasi kwani uwasilishaji wa fomu za matokeo ya uchaguzi wa urais ulicheleweshwa huku ikiwataka wadau kusimamia amani hadi mchakato huo utakapokamilika.

Watakaoficha chakula kushakiwa kwa uhujumu uchumi
Dkt. Mwinyi asifu amani mikutano ya hadhara, akemea upotoshaji