Irene Uwoya usiku wa kuamkia leo aliwasapraizi mastaa na mashabiki wake kwa kuwaalika kwenye tukio ambalo hata hivyo kwa mujibu wao hadi wanafika ukumbini jijini Dar es Salaam hawakuwa wanajua nini hasa kinachoenda kufanyika.

Msanii huyo aliyepata nafasi kwenye mkondo ‘A’ wa tasnia ya maigizo kupitia filamu ya ‘Oprah’ aliwapa kitu cha tofauti wakiwa ndani ya ukumbi huo, baada ya kuweka wazi kuwa ni maandalizi na uzinduzi wa kipindi cha maisha yake halisi (Reality TV Show) kilichopewa jina la Hail To The Queen.

Kati ya watu maarufu waliohudhuria na kuzungumza kwenye tukio hilo ni pamoja na Elizabeth Michael (Lulu) na Diamond Platinumz.

Lulu alimpongeza Uwoya kwa alichokifanya na kueleza kuwa hatua hiyo imewafungulia njia waigizaji kama yeye hasa wa kike ili waanze kufikiria nje ya box.

“Nakutakia kila la kheri, umetufungulia na sisi, pengine tunaweza.. [inawezekana] tusije na ‘reality shows’ lakini tutaanza kufikiria katika jicho la tatu, sio kwamba tufanye tu movies, sio kwamba tuwe tu video vixens, tunaweza kufanya mengi kwa vipaji vyetu,” alisema Lulu.

Irene Uwoya na mwanaye Krish wakisikiliza jumbe za watu maarufu

Kwa upande wa Diamond, yeye alionesha kuridhishwa na ubora wa tukio hilo na bidhaa iliyozinduliwa, akapongeza. Lakini aliwapa ujumbe mzito wasanii wa kike nchini akiwataka kuamka kwani Watanzania wamechoka kusikia wasanii wa Nigeria wakifanikiwa wakati anaamini tunao wasanii bora zaidi yao.

“Mimi nawapongeza sana na nawatakia kila la kheri, na naamini kupitia yeye dada zetu wengine pia watajifunza vitu tofauti. Tumeshachoka kuona akina Genevieve Nnaji wanafanya vitu vikubwa halafu dada zetu wanaonekana kama hawafanyi vitu. Kwa sababu kwanza tunaamini dada zetu wazuri kuliko wao… wana nyota kuliko wao, na kama madanga tunao kuliko wao,” alisema Diamond Platinumz.

Msanii huyo pia alimpa furaha ya kipekee mtoto wa Uwoya, Krish ambaye alisema kuwa ndoto yake ilikuwa kukutana naye kwa sababu anapenda anavyoimba; na anatamani siku moja amfundishe kucheza.

‘Hail to The Queen’ imezinduliwa usiku wa kuamkia leo saa chache baada ya kuwepo tetesi nyingi kuwa Irene Uwoya amefunga ndoa kwa mara ya tatu.

Asimulia penzi la usiku mmoja lilivyomponza, 'wasichana bebeni mipira kwenye mikoba yenu'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 27, 2019