Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amewataka wabunge kuwacha kukaa kwenye kiti cha Waziri mkuu mda mrefu na wamuache asikilize hoja za wabunge kwani yeye ndiye msimamizi wa shughuliza Serikali Bungeni.

Amesema hayo leo leo Juni 17, 2021, Bungeni Dodoma wakati wa majadiliano ya Bajeti, na kueleza kuwa hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara na kwamba kuanzia leo ataanza kuwachukulia hatua.

Aidha Dkt Tulia ameonesha kutokufurahishwa na jinsi ambavyo wabunge wa Bunge hilo wanavyopiga kelele ndani ya Bunge hata kama kuna mwenzao anatoa hoja.

“Waheshimiwa wabunge mliosimama naomba mkae, wabunge mnapiga kelele sana mimi huletewa malalamiko lakini huwa sipendi sana kuwaambia keleleni, sababu watu wanasikiliza na wamekuja hapa Bungeni kujifunza, tujizuie kuongea kwa sauti kama upo nje, pia anayechangia hapa wewe msikilize ili hoja uielewe,” amesema Dkt. Tulia.

“Kuna wengine mnaenda kwenye kile kiti (Kwa Waziri Mkuu), yeye atasikiliza saa ngapi hoja za wabunge? na yeye ndiyo msimamizi wa shughuli za serikali Bungeni kwa hiyo tafadhali, sasa hivi nikiona mtu pale amekaa muda mrefu nitakunyanyua,” amesisitiza Dkt. Tulia.

Ujenzi daraja la Tanzanite wafikia asilimia 83.5
Mkosoaji wa Kagame afungwe maisha