Serikali sasa inatarajia kuokoa shilingi Bilioni 22.4 kwa mwaka ambazo zilikuwa zikigharamia ununuaji wa mafuta kuendeshea mtambo wa Jenereta na matengenezo yake, ili kupata umeme uliokuwa ukitumika Mkoa wa Kigoma.

Uokoaji wa kiasi hicho cha pesa unafuatia Mkoa huo kuunganishwa katika umeme wa Gridi ya Taifa ambapo tayari TANESCO Septemba 17, 2022 kuzima rasmi majenereta yaliyokuwa yanazalisha umeme yaliyopo Kibondo na Kasulu.

Ujenzi wa Mitambo ya umeme.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema, kupatokana kwa umeme huo wa gridi ya Taifa, kutasaidia pia kuondoa changamoto zilizokuwa zikilikabili eneo la Ngara na Kagera kwa kupakana kwa umeme wa uhakika, ambapo hapo awali yalikuwa yakipata umeme mdogo.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, Mkoa wa Kigoma sasa rasmi umeunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa na tayari TANESCO imezima rasmi majenereta yaliyokuwa yanazalisha umeme kwa ajili ya Mkoa huo.

Samia, Ruto watumia basi maalum Mazishi ya Malkia
Kamishna Nyanda akagua miradi ya TAWA