Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa agizo la kuhamisha wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda Hospitali ya Tiba na Taaluma Mloganzila.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuangalia hali ya utoaji wa huduma pamoja na utekelezaji wa agizo hilo alilolitoa wakati alipotembelea Hospitali ya Tiba na taaluma Mloganzila mapema mwezi huu.

“Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa waliopo kwenye jengo la Mwaisela kuanzia wodi namaba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa wagonjwa mahututi na wenye kesi maalumu ila nawapongeza wametekeleza agizo hilo mara moja” amesema Ummy.

Aidha, amewapongeza MNH kwa kuwahamisha madaktari bingwa 15 na wauguzi zaidi ya 30 kwenda katika Hospitali ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma sawa na inayotolewa Muhimbili.

Hata hivyo, ameongeza kuwa zoezi hilo limetoa nafasi ya kuwahamisha baadhi ya wagonjwa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) hususani watoto angalau vitanda 50 kupeleka kwenye jengo la Mwaisela hospitali ya MNH.

 

Young Africans washindwa kutamba nyumbani
Aliyewadunga wanawake ‘mimba feki’ atiwa mbaroni