Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans, wameshindwa kutamba katika uwanja wa Uhuru kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana na Mwadui FC waliofunga safari kutoka wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Young Africans walikua wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo, kutokana na makosa waliyoyafanya katika mcezo uliopita dhidi ya Mbao FC na kusababisha kufungwa mabo mawili kwa sifuri jijini Mwanza mwishoni mwa mwaka jana.

Katika mchezo wa leo Young Africans ilimtumia mshambuliaji kutoka nchini Burundi, Amissi Tambwe ambaye ametoka kuugua Malaria huku ikiwaacha benchi chipukizi kama Yohanna Oscar Nkomola na Said Mussa ‘Ronaldo’ walio fiti matokeo yake safu yake ya ushambuliaji ikawa butu leo.

Tambwe alionekana kabisa hayuko fiti, kwa sababu alicheza chini ya kiwango na akaikosesha timu nafasi kadhaa za kufunga.

Safu ya ushambuliaji ya Young Africans ilichangamka na kuanza kulitia misukosuko lango la Mwadui baada ya kuingia chipukizi Said Ronaldo na Nkomola waliokwenda kucheza pamoja na kaka yao Ibrahim Ajib pale mbele. Bahati mbaya, Ajib naye leo hakuwa katika ubora wake.

Young Africans ilifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Mwadui FC, lakini ikashindwa kupata bao kutokana na wageni kuamua kucheza kwa kujihami mwishoni mwa kipindi cha pili.

Kipindi cha kwanza Mwadui ikiongozwa na mshambuliaji wake mkongwe, Paul Nonga ilitawala mchezo na kipindi cha pili Young Africans walizinduka na kuuteka mchezo lakini hadi dakika 90 zinamalizika mambo yalikua magumu kwa pande zote mbili.

Matokeo ya bila kufungana  yanazidi kuitoa Young Africans kwenye mbio za ubingwa, ikifikisha pointi 22 baada ya kucheza michezo 13, sasa wakizidiwa pointi nne na vinara Simba na Azam FC ambao pia wana mechi moja moja mikononi.

Simba watateremka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kumenyana na Singida United wakati, Azam FC watakuwa Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kumenyana na wenyeji, Maji Manji katika mchezo wa kukamilisha mzunguko wa 13 wa Ligi Kuu.

Dkt. Abbas awataka waandishi kugeukia maendeleo kuliko siasa
Ummy Mwalimu aridhishwa na kasi Muhimbili