Wakati Waislam nchini kote wakiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Kampuni ya Simu Ya Mkononi Airtel kupitia huduma zake za kijamii yaani Airtel FURSA, wametoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa vituo viwili vya yatima jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Bw,Jackson Mmbando alisema ’’Huo ni mwendelezo wa  huduma za kujitolea  kwa jamii za Airtel kwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakati wa mfungo ambapo  kwa mwaka huu msaada utafika kwenye vituo 10’’

Tanzania Yagundua Hifadhi Kubwa Yenye Gesi Adimu, Rasilimali Zinawasaidiaje Watanzania?
Aenda Jela kwa Kudanganya Kwenye Mtihani India, Sheria hii Ianze Tanzania?