Muigizaji  maarufu kutoka  nchini Kenya  Lupita Nyong’o  ameweka rekodi nyingine  kwenye mauzo  ya filamu mpya  ya US iliyoachiwa rasmi Machi 8,2019, baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Black Panther iliyotoka Februari mwaka jana.

Katika filamu hiyo mpya Lupita amecheza kama Mhusika mkuu (Main Character), imeweza kuingiza jumla ya dola za Kimarekani 70.2 millioni sawa na bilioni 165 za Kitanzania.

Aidha filamu hiyo imevuka lengo la makisio ambapo ilitabiriwa kuingiza kiasi cha ($68 millioni) sawa na Tsh bllioni 159 kabla haijatoka.

Imeelezwa kuwa filamu ya US imeongozwa na kuandikwa na Jordan Peele, iliachiwa kwa mfumo wa Trailer na ilitengenezwa kwa bajeti ya dola millioni 20 za kimarekani sawa  na Zaidi ya billioni 46 za kitanzania.

Kutokana na mauzo hayo filamu ya US inatajwa  kuwa filamu ya kutisha iliyouza Zaidi Dunianai  kwenye wiki ya kwaza kwa muda wote

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=1tzFRIQfwXg]

 

 

Jengeni tabia ya kupima afya mara kwa mara- Samia Suluhu Hassan
Ndege nyingine ya Boeing yatua kwa dharura