Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema anampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Roggers Siang’a kwani kwa kufanya hivyo ataweza kufanikiwa kukabiliana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Ameyasema hayo leo katika Ibaada iliyofanyika Kanisani kwake Ubungo Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli ameona mbali ndiyo maana ameamua kufanya uteuzi huo.

Aidha, Gwajima amesema kuwa hatamfungulia mashtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kwa kuwa akifanya hivyo atakuwa ameishtaki Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ameamua kwenda kumshtaki kwa Rais ili amshughulikiwe yeye mwenyewe.

Vile vile, Gwajima ameongeza kuwa hata kama watu wanajihusisha na biashara za madawa ya kulevya, huwezi kutumia utaratibu huo wa kuwatangaza kwenye vyombo vya habari kwani utakuwa uanapoteza ushahidi na kuwachafualia majina yao.

Hata hivyo, Gwajima amemuomba Rais Dkt. Magufuli amewaombea msamaha Maafisa Polisi waliokamatwa ambao wamewekwa chini ya ulinzi zaidi ya wiki mbili huku wakiwa wamesimamishwa kazi.

Pia amesema kuwa yuko tayari kuwakatia  rufaa watu wote waliowekwa ndani kwa tuhuma za madawa ya kulevya,hivyo ameomba wapelekwe mahakamani na si kuendelea kukaa mahabusu.

JPM amkabidhi Majaliwa pambano madawa ya kulevya
Kamishna mpya wa madawa ya kulevya kuwatia mbaroni wote wanaohusika