Kwa muda mrefu tangu Harmonize kujiengua katika kundi la WCB hajaweza kudondosha ngoma aliyoifanya peke yake.

Mapema leo Oktoba 24, 2019 Konde boy ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la Uno ambapo katika ngoma hiyo kwenye moja ya mstari amemtaja aliyekuwa boss wake Chibu Dangote na aliyewahi kuwa mpenzi wake na kumzalia Chibu watoto wawili, Zaritheboss lady.

Ni ngoma ambayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa wa Instagram amekuwa akiwaandaa mashabiki zake kwa hamu zote kusubiri ujio wake kwa kuifanyia promo na kuitambalisha kwa namna mbalimbali.

Hadi sasa ngoma hiyo imekwisha sikilizwa na watu takribani 64,830, sikiliza hapa chini.

Samia mgeni rasmi semina wabunge wanawake Jumuiya ya Madola
DC Mjema amjibu RC Makonda