Msanii wa nyimbo za Asili nchini, Mrisho Mpoto amesema kuwa huu si wakati wa kutupiana lawama katika suala zima la ukuzaji wa lugha ya kiswahili bali ni wakati wa kushikamana ili kuikuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa fainali za shindano la sauti lililofanyika jijini Dar es salaam, ambapo washindi kumi wa sauti watasafirishwa kwenda China na Kampuni ya Startime
“Huu si wakati wa kulaumiana na kunyoosheana vidole, tunatakiwa kushikamana ili kuweza kukuza lugha yetu, tuitangaze kimataifa ili iweze kupenya zaidi katika mataifa mbalimbali,”amesema Mpoto.