Nguli wa Bongo Fleva, Ambene ‘AY’ Yesaya ameweka wazi kuwa bifu kati ya swahiba wake Mwana FA na Lady Jaydee iliyofukuta mwaka 2013 ilimpa wakati mgumu.

Mkali huyo wa mtindo wa ‘Commercial’ amesema alipata wakati mgumu kuona wasanii hao hawazungumzi wakati wote ni rafiki zake lakini aliamini siku moja wataufunga ukurasa wa uhasama huo.

AY aliiambia EATV kuwa hivi sasa anafurahi kuona wawili hao wamefunga kweli ukurasa huo na wanazungumza kama ilivyokuwa awali.

“Mimi nilikuwa napata wakati mgumu sana, kwasababu hawa hawaongei alafu wote washkaji, lakini ikafika time (muda) wakawa wanauliziana. Nikajua sasa hivi watakuwa sawa,” AY alifunguka.

Kabla ya kukwaruzana mwaka 2013, AY na FA waliwahi kufanya kazi pamoja mara kadhaa. Moja kati ya ngoma waliyofanya pamoja iliyoteka mitaa ni ‘Alikufa Kwa Ngoma’, ‘Hawajui’, ‘Msiache Kuongea’, ‘Wanaume Kama Mabinti’.

Video: Sarkodie na Korede Bello wakutana kwenye 'Far Away'
Video: JPM awapa ‘neno’ waliovunja nyumba ya CCM