Baada ya kutokea majanga makubwa ya kimbunga katika kisiwa cha Puerto Rico chenye watu milioni 3.5 na kusababisha uharibifu wa miundo mbinu tukio hilo limewafanya baadhi ya watu mashuhuri kujitolea fedha kwa ajili ya kukijenga upya kisiwa hicho.

Mmoja kati ya watu walioguswa ni mwanamuziki Jennifer Lopez ambaye ameamua kujitolea dola milioni 1 kwa ajili ya kusaidia Puerto Rico pesa hizo zikiwa zinatoka kwenye show zake anazozifanya huko Las Vegas Marekani.

J Lo ambaye wazazi wake wanametokea katika kisiwa hicho alitoa taarifa hiyo kupitia mkutano ulioudhuliwa na gavana wa New York Andrew Cuomo uliofanywa mahususi kwa ajili ya kuisaidia Puerto Rico.

Tazama video ya J lo akiwa kwenye mkutano wa kuhamasisha kuichangia Puerto Rico

Mwakyembe: Nataka mkandarasi mpya wa kutoa tiketi uwanja wa taifa utakapofunguliwa
DC na RC waonywa utumiaji mbovu wa madaraka