Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kupata eneo la kujenga Shule ya Msingi katika eneo la Mbagala Mbande ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Mbande.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara yake wilyani humo ya kukagua mpango mkakati wa wilaya hiyo katika ujenzi wa shule na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, Makonda amewataka watumishi wa Serikali katika Idara mbalimbali kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zilizotengwa katika bajeti ili kutekeleza miradai ya maendeleo wilayani humo hususani katika sekta ya elimu.

“Nataka kila mtumishi katika idara awe mtu wa kutatua changamoto za wananchi na si kutengeneza migogoro  katika idara yako, kama unaona pesa ulizotengewa katika bajeti ni kiasi kidogo, mbane mkurugenzi akuongeze ili uweze kutimiza malengo na miradi ya idara yako siyo kukaa ofisini na kusubiri tu,”amesema Makonda

 

Video: Saa 120 za patashika msiba wa Akwilina, Chadema yazidi kubomoka
Edgar Lungu azitaka nchi za Afrika kutokomeza ukoloni