Belle 9 ameachia rasmi video ya wimbo wake ‘Give It to Me’ aliyomshirikisha Mweusi G-Nako.

Video ya wimbo huu imefanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Nicroux. ‘Give It to Me’ ni moja kati ya nyimbo za mkali huyo kutoka Morogoro ambazo zitapatikana kwenye albam yake mpya ya ‘Vitamin Music Volume 1, The Year of Belle 9’, itakayotoka mwaka ujao.

Hii ni kazi yake ya kwanza akiwa chini ya uongozi mpya wa ‘Vitamin Music Group’.

Mugabe achaguliwa kugombea tena urais 2018
Serikali kuwasha umeme vijiji vyote nchini mwakani