Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kuwa vijiji vyote nchini vitafikiwa na umeme kufikia Aprili mwakani ikiwa ni sehmu ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA).

Akizungumza jana na watendaji wa idara za Serikali wilayani Longido, ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Arusha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kuwa tayari Serikali imeshasaini mkataba na wakandarasi watakaounganisha umeme katika vijiji 8,000 vilivyosalia katika awamu ya kwanza na ya pili ya mradi huo.

Waziri Mkuu alisema kuwa utekelezaji wa ahadi hiyo utakamilika Aprili mwakani na kwamba kwa vijiji ambavyo havitafikiwa na umeme wa gridi ya taifa wataunganishiwa umeme wa nishati ya jua kwa gharama ya kawaida ya shilingi 27,000.

Alisema kuwa nishati hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaoishi vijijini kujikwamua kiuchumi kwa kubuni miradi zaidi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jumaa Mhina kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa na hospitali ya wilaya.

Video Mpya: Belle 9 Feat. G Nako – Give It to Me
Gari la Sugu lilivyochukua maisha ya mtoto yatima