Mbunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Abdallah Mtolea amesema kuwa, Profesa Lipumba hana uwezo wa kumkaimisha mtu cheo chochote kwa sababu Katiba ya chama hicho hairuhusu.

Mtolea amesema hayo wakati akizungumza na Dar24, ambapo ameeleza kuwa Prof. Lipumba hana uwezo wowote kwa sababu Katibu anachaguliwa na Mkutano Mkuu wa kitaifa na kuongeza kuwa Magdalena Sakaaya hawezi kukaimu nafasi hiyo kwakuwa Katibu Mkuu yupo na anafanya kazi zake kama kawaida.

“Katibu Mkuu yupo, tunamshangaa Lipumba kwa kumkaimisha Magdalena Sakaaya, hilo jambo halipo na anachokifanya ni kujidhalilisha  tu,”amesema Mtolea.

Hata hivyo, Mtolea ametoa ushauri wake kwa Prof. Lipumba na kumtaka apumzike aachane na masuala ya siasa ili azidi kulinda heshima yake.

FA Yaibana Manchester City, Yatoa muda hadi Alhamisi
Eden Hazard Kuikosa Ugiriki