Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha, Isaya Doita amesema kuwa hakuna maendeleo yeyote yanayofanywa na rais Dkt. Magufuli

Ameyasema hayo Jijini Arusha alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema haoni maendeleo yanayofanywa na rais Dkt. Magufuli na kuwashukia wanaohama Chadema akisema wananunuliwa.

Amesema kuwa Chadema ni chama imara na chenye ushindani mkubwa hivyo, haoni haja ya kuhama na kuunga mkono juhudi za rais Dkt. Magufuli.

“Siwezi kuhama Chadema kwasababu sioni maendeleo yeyote yanayofanywa na serikali ya awamu hii ya tano, na wanaohama wanahamishwa na njaa zao,”amesema Doita

 

 

Tottenham kuikaribisha Man City Wembley Stadium
Carlos Osorio kocha mpya Paraguay