Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amesema watanzania wanapenda elimu ‘mserereko’ yaani vijana wanaoanza shule darasa la kwanza mpaka kufika kiwango cha PHD bila kupitia ujuzi wa kazi yoyote.

Mwijage amesema kuwa kimsingi elimu yake ya darasani ni ndogo, aliyonayo ni elimu ya mtaani na imemsaidia kwani amefanya kazi nyingi sana tofauti na wale waliosoma elimu ‘mserereko’ ambayo imekuwa tatizo kubwa.

“Kimsingi mimi elimu ya darasani ni ndogo, niliyonayo ni elimu ya mtaani nimefanya kazi nyingi, nimevua samaki, nimefanya kazi garage, niwahi kuwa hata DJ, hii elimu mseleleko hujawahi kufanya kazi yoyote, unakuwa injinia, kwa hiyo kijana ukikwama tafuta namna unavyoweza kuanza” – Waziri Mwijage

Video: Ali Kiba aeleza kwanini hajikiti kusaka collabo za kimataifa
Kanye West awatishia nyau waandaaji wa tuzo za Grammy