Wizara ya afya inaisihi jamii kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia yafuatayo:

  • Utoaji na upatikanaji wa takwimu sahihi za ugonjwa kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara bila kuingiliwa na viongozi wa ki siasa au kiserikali.
  •  Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo yote ya mjini na vijijini ili kupunguza hatari ya kuenea kwa ugongwa huu.
  •  Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kupitia Mamlaka za maji zilizopo katika ngazi zote.
  •  Kuhakikisha utunzaji salama wa maji ya kunywa yaliyotibiwa.
  • Kuwahi kupata matibabu mapema katika vituo vya kutolea huduma.
  • Kuhakikisha upatikanaji na matumizi sahihi ya ORS katika maeneo mbali mbali nchini ili kupunguza athari za ugonjwa.

Video: Makonda awapa wiki mbili Wakuu wa Wilaya kutengeneza Mpango kazi
Kipindupindu Kupungua Nchini, Morogoro Bado Changamoto