Jitihada mbalimbali  zinazofanywa na Serikali kuhakikisha ugonjwa  wa kipindupindu unamalizika nchini zimefanikiwa na  kueleza kuwa mpka sasa mkoa ambao bado unaripoti ya kuwa na ugonjwa huo ni Morogoro tu.

Ugonjwa wa kipindupindu ulianza takribani miezi kumi sasa iliyopita  ambapo takribani watu 345 wamepoteza maisha huku wagonjwa 22,216 walitolewa taarifa ya kuugua ugonjwa huo.

Taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, kwa wanahabari inasema changamoto za kukabiliana na ugojwa wa Kipindupindu ni kubwa lakini ugonjwa  huu ulioanza Agost 2015 unakaribia kuisha huku akisistiza jitihada za ziada zinahitajika Mkoani Morogoro ili kuhakisha ugonjwa huu unapotea nchi nzima.

Aidha katika hali ya sasa ya kuwa na wagonjwa wachache, ametoa agizo kwamba wagonjwa wote wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu wa kipindupindu wathibitishwe kwa vipimo vya maabara na kupatiwa matibabu .

”nasisitiza kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kutotoa taarifa sahihi za wagonjwa wa Kipindupindu na magonjwa mengine ya mlipuko”Amesema Mh.Ummy.

 

 

 

Vidokezo Muhimu vya Kupambana na Kipindupindu
Video: 'Full Interview' ya Ibrahimovic Manchester United