Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Meshack Chinyuli amesema katika kuhakikisha huduma za uratibu wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii zinaendelea kuimarika, Serikali ina mpango wa kutumia mfumo wa Kidijitali.

Dkt. Chinyuli ameyasema hayo Mkoani Morogoro wakati akizungumza Kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wadau chenye lengo la kutengeneza mkakati wa pamoja wa kuimarisha Afua za Afya ngazi ya Jamii, ambapo pia watajadili mikakati ya pamoja ambapo amefafanua kuwa mfumo wa Teknolojia na wa Kidijitali utakuwa na mchango mkubwa katika uratibu wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Kwa upande wake Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. May Alexander amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wamepata Mafunzo rasmi na wanalenga maeneo makuu matatu ikiwemo masuala ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe huku John Yuda kutoka Wizara ya Afya akisema Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii wana mchango mkubwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Subiya Kabuje amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii husaidia kuibua viyendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo walemavu waliofichwa nyumbani pamoja na kuibua wagonjwa hivyo wana mchango mkubwa katika Jamii .

Madereva, Wamiliki Mabasi ya shule watahadharishwa
TAKUKURU yaongeza mapato machinjio ya Mtakuja