Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imebaini uzembe katika kusimamia idadi ya ng’ombe wanao chinjwa kwa siku husika na hakuna ukaguzi kuhusu idadi ya Ng’ombe waliopo eneo la kusibiri kuchinjwa, katika machinjio ya Mtakuja yaliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Ally Sadiki akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari amesema, chambuzi huu umefanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba kuna miaya ya rushwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ushuru katika machinjio hayo, hali inayodababisha upotevu wa mapato na Halmashauri.

Amesema, “uchambuzi huu umebaini kwamba pamoja na kuwepo kwa mashine za kieletroniki za POS katika machinjio kumekua na taarifa zinazokinzana ,kuwepo kwa tatizo la miundombinu na ucheleshaji wa kuweka fedha benki zinazo kisanywa, pia kuna uzembe katika kusimamia idadi ya ng’ombe wanao chinjwa kwa siku husika na hakuna ukaguzi kuhusu idadi ya ng’ombe waliopo eneo la kusibiri kuchinjwa.”

Aidha, Sadiki ameongeza kuwa baada ya TAKUKURU kuingilia kati makusanyo yameongezeka tofauti na ilivyokua katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kati ya Oktoba na Desemba 2023 ambapo Oktoba hadi Desemba makusanyo yalikua Mil. 7,418,000 na sasa makusanyo yameongezeka na kufikia kiasi cha Mil. 9,615,000.

Ameongeza kuwa, TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 23 yenye thamani ya Bilioni 6.3 katika sekta za Elimu, Maji, Afya na Ujenzi (Barabara), ambapo kati ya miradi hiyo mradi mmoja umeonekana kuwa na upungufu ufuatiliaji unaendelea ii kurekebisha kasoro hizo.

Mfumo Kidijitali kurahisisha huduma za Afya ngazi ya jamii
Van Dijk: Tunapaswa kusahau na kusonga mbele