Serikali nchini Uganda, imepeleka wanajeshi wake mpaka wa Mpondwe unaotenganisha eneo lake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya shambulizi la kigaidi kwenye Kanisa ambapo watu 17 walifariki Januari 15, 2023.
Kwa mujibu wa tarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Kasese inayopakana na Kongo, Joe Walusimbi iliyochapishwa kwenye gazeti moja la kila siku nchini humo, imesema wanajeshi hao wanachunguza mienendo ya waasi wa ADF wanaotaka kuvuka mpaka.
Awali, Msemaji wa Jeshila Polisi nchini Uganda, Fred Enanga alisema kumekuwepo na utekelezwaji wa operesheni za usiku zenye kuleta mashaka, ambazo zimekuwa zikifanywa kwenye meli za mizigo na abiria katika ziwa Albert.
Mamepa mwezi Desemba, 2022, Uganda iliwakamata watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa ADF, waliovuka mpaka na kuingia katika Wilaya ya magharibi mwa nchi hiyo Ntoroko.