Watanzania, wameombwa kuungana katika kupiga vita vitendo mmonyoko wa maadili hasa vitendo vya ushoga, ulawiti na usagaji ambavyo vimeonekana kushamiri kwenye baadhi ya jamii za Kitanzania ili kulinda maadili na utu.
Akihutubia waumini wa kiislamu katika baada ya swala ya Eid Al-Fitri iliyoswaliwa leo April 22, 2023 katika uwanja wa shule ya Msingi Kashato, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Nassoro Kakulukulu amesema viongozi wa dini wanaunga mkono juhudi zilizoonyeshwa na wabunge kukemea suala hilo la ushoga, ulawiti na usagaji.
Amesema, ‘”ikiwa wanawake wataoana wao kwa wao wanasagana na wanaume kuoana wao kwa wao kizazi kitaongezeka vipi? ni lazima kila mmoja wetu tukemee jambo hili kwa nguvu zetu zote” na sisi kama viongozi wa Dini tunayasema haya kwa kuwa wanaoathirika na vitendo hivyo ni watoto wadogo hivyo kila mtu ni lazima kuchukua tahadhari juu ya matendo hayo maovu.”
‘’Wapo watoto wa miaka kumi, miaka 5 ambao tayari wameshaharibika kwa hiyo tusipoyasema haya watoto hawa tunawaweka katika mazingira magumu, watoto wapo mashuleni wamekwishaharibika na sisi wazazi tuhakikishe watoto wetu waliopo mashuleni tunawafatilia vilivyo, wale wanaosoma shule za boarding (bweni) tuwafatilie vizuri ’’ amesisitiza Sheikh Kakulukulu.
Aidha katika hatua nyingine ameeleza kuwa ikiwa kutakuwa na Mpango maalumu wa kupima ili kuwabaini Mashoga viongozi wa Dini ya kiislamu katika mkoa wa Katavi watakuwa wa kwanza kupima ikiwa ni sehemu ya Mapambano juu ya swala hilo.
“Kwahiyo likija suala la kupimwa ili kuwabaini wanaojihusisha na masula ya ushoga sisi viongozi wa Dini wa Kiislamu na Dini ya Kikirsto tujitokeze twende tukapime ili pumba na mchele ujulikane, tunaweza tukachanganyikana kwa kupinga ushoga kumbe wewe mwenyewe ni shoga,’’ amesema Sheikh Kakulukulu.