Wezi wa mali za Umma wameanza kukiona cha ‘mtema kuni’ katika baadhi ya nchi barani Afrika kutokana na mabadiliko ya uongozi unaoingia madarakani kwa kasi.

Nchini Nigeria, viongozi waliowahi kuiba mali za umma wameanza kujisalimisha na baadhi yao kurejesha kwa hiari mali walizoiba ili balaa lisiwaangukie.

Buhari

Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari amebainisha wiki hii kuwa wanaendelea kupitia nyaraka zote za serikali ili kuwabaini wezi wote na kwamba watawafikisha mahakamani mara moja.

“Maafisa waliopita waliwabia watu wasio na hatia. Lakini tumeanza kupitia nyaraka zote na baadhi yao wameanza kurejesha kitu kwa hiari. Lakini tunataka warejeshe wote,” alisema Buhari na kusisitiza kuwa watawaonesha wananchi wezi wao.

Picha: IS Watoa Picha Ya Mtu Aliyelipua Gari La Walinzi Wa Rais Wa Tunisia
Mtatiro Aikosoa kwa nukuu ya sheria, Amri ya Makonda kuwaweka selo maafisa waliochelewa kazini