Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limewateua waamuzi kutoka nchini Misri, kuchezesha mchezo wa tatu wa kundi “A” wa kombe la shirikisho kati ya mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans dhidi ya Medeama ya Ghana, uliopangwa kufanyika Julai 16 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ibrahim Nour El Din amatajwa na CAF kuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad.

Mohamed Maarouf Eid Mansour atakuwa mwamuzi wa akiba.

Raia wa Zambia, Pasipononga Liwewe atasimama kama kamisaa, Mfubusa Bernard kutoka Burundi atakuja kama mkaguzi wa waamuzi huku Ian Peter Keith Mc Leod kutoka Afrika Kusini ndiye mratibu mkuu wa pambano.

Jambazi aliyetoroka Mwanza aibua hofu, Wizi wa fedha za Umma SMZ ni kigugumizi
Juventus Kumuuza Paul Pogba Kwa Masharti