Zaidi ya wanajeshi 80 wa Yemen wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa kwenye Shambulizi la Kombora la Ndege zisizokuwa na Rubani lililofanywa na Waasi wa Houthi katikati ya Yemen.

Mashambulizi hayo yanafuatia miezi kadhaa ya utulivu kiasi katika Nchi hiyo inayokabiliwa na vita kati ya Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Waasi wa kihouthi walishambulia msikiti mmoja katika Kambi ya Kijeshi iliyoko kwenye mkoa wa kati wa Marib kilomita 170 Mashariki mwa Mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Magharibi.

Mashambulizi yamefanyika siku moja baada ya wanajeshi wa Serikali wanaoungwa mkono na Kikosi cha Muungano kuanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wahouthi katika mkoa wa Nihm Kaskazini mwa Sanaa.

ACT kupinga Mahakamani Serikali kufunga laini za simu
Rukwa: Hofu yazidi, wazazi wawapa watoto dawa za kupanga uzazi

Comments

comments