Maelfu ya wafanyakazi wa umma nchini Afrika Kusini, wameingia katika mgomo wa kitaifa kuhusu mishahara baada ya mazungumzo na serikali kugonga mwamba hali ambayo imetishia kuathiri huduma muhimu.

Mgomo huo, uliongozwa na vyama vikubwa zaidi vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini hasa Chama cha Watumishi wa Umma (PSA), ambacho kina wanachama zaidi ya 235,000.

Mkwamo wa mishahara ya wafanyakazi uliongezeka baada ya Waziri wa kazi, Thulas Nxesi wiki jana kutangaza kwamba atatekeleza nyongeza ya asilimia tatu kwa upande mmoja katika bodi nzima wakati vyama vya wafanyakazi vinataka ongezeko la asilimia 6.5.

Wafanyakazi wa umma nchini Afrika Kusini, wameingia katika mgomo wa kitaifa kuhusu nyongeza ya mishahara. Picha ya Twitter.

Wanachama wa vyama vya wafanyakazi wakiwemo wauguzi, Uhamiaji na baadhi ya maafisa wa Polisi waliochukuliwa nje ya ofisi ya Hazina ya Pretoria waLipeperusha mabango meusi yaliyosomeka “watumishi wa umma wanavuja damu” huku PSA ikionya kwamba mgomo huo ungekuwa na athari kwa idara ya mambo ya ndani, uchukuzi na udhibiti wa mipaka.

Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Enoch Godongwana alisema wakati wa hotuba yake ndogo ya bajeti ya Oktoba kwamba serikali inaweza kumudu tu nyongeza ya wastani ya mishahara ya asilimia 3.3 huku ongezeko hilo likiwa na uzito chini ya mfumuko wa bei wa Afrika Kusini ambao ulifikia asilimia 7.8 mwezi Julai (2022).

Uchumi wa Taifa la Afrika ya Kusini, hivi karibuni ulipata pigo wakati wafanyakazi katika kampuni ya Reli ya Serikali na Bandari, walipoanzisha mgomo wa wiki moja iliyopota ambao pia uliacha mauzo ya madini na matunda kukwama.

Ajali: Lori la Saruji lagonga magari Tegeta
Kamati ya uokoaji 'yakuna kichwa' tishio baa la njaa