Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Nadal Al-Nashif na ujumbe wake Ikulu Zanzibar hii leo Machi 9, 2024.

Dkt. Mwinyi amesema Zanzibar itaimairisha ushirikiano katika kujenga uwezo Taasisi za kisheria hususani utekelezaji wa sheria, Mahakama na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.

Naye Naibu Kamishna, Nadal Al-Nashif amesema wataisaidia Zanzibar katika kuwajengea uwezo hususani Taasisi za kisheria.

Hata hivyo, atika mazungumzo yao wamezungumzia nafasi ya Vyombo vya Habari, huduma za maendeleo ya kijamii, utalii, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na uwezeshaji wa Wanawake na Vijana.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 10, 2024
Kishindo kipya teuzi, mabadiliko Wakuu wa Mikoa, Wilaya