Mamiloni ya wanawake nchini India hawajawahi kuwaita waume zao kwa majina yao ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha heshima na kudumisha mila na tamaduni zao.

Tamaduni hiyo inaheshimika na kufuatwa zaidi vijijini licha ya kutokuwepo sana mijini, hivyo wapo wanaopinga tamaduni hiyo na kuanzisha kampeni wakishauri wanawake vijijini kuachana na tamaduni hiyo.

Kwa utamaduni wa India, bwana/mume ni sawa na miungu hivyo mabinti huanza kufunzwa kumuheshimu wakiwa na umri mdogo.

Mabinti hufunzwa kumuita mume kwa jina lake inaweza kumletea bahati  mbaya na kupunguza maisha yake, kuvunja tamaduni hiyo pia kunaweza kumletea mwanamke adhabu kali. Mwanamke mmoja katika jimbo la Orisa amewahi kuadhibiwa vikali baada ya kuvunja tamaduni hiyo.

Nini maoni yako kuhusu tamaduni kama hizi, je mwanaume ni kweli anaheshimiwa kwa kutotajwa jina lake?

Jafo awatahadharisha watumishi wa umma
Tanesco waigomea bomoabomoa Kimara