Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imewahukumu kifungo cha kunyongwa mpaka kufa watu 3 baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia.

Akitoa hukumu hiyo Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Dkt. Adam Mambi amewataja waliohukumiwa kuwa ni Nathani Elias (31), Moses Kasitu (26) na Eliasi Mzumbwe (23).

Amesema adhabu hiyo ni fundisho kwa vijana wengi wanaotumia njia za mkato kupata fedha zisizo za halali, na kusababisha mauaji yanayomaliza nguvu kazi ya taifa .

Akisoma shauri hilo mahakamani hapo Wakili wa Serikali, Shindani Michael amesema washitakiwa wametenda kosa hilo Julai 25, 2014, eneo la Mpemba katika Halmashauri ya Mji Tunduma uliopo wilayani Momba mkoani songwe.

Amesema washitakiwa hao walimvamia marehemu Vascal Njowela, akiwa ametoka dukani kwake akielekea kwa bosi ili kuwasilisha mauzo, ambapo alikutana na watu hao watatu waliompiga risasi na kumkata kwa mapanga wakitaka kupewa Milioni 1, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya East Afrika.

Patrick Aussems amuhofia Meddie Kagere
Nikki Mbishi ampongeza harmonize kutoka WCB