Wamiliki wa mtandao wa Twitter wamefanya operesheni dhidi ya akaunti zote zinazosadikika kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la IS na kuziondoa.

Twitter wameeleza kuwa operesheni hiyo imefanikisha kufuta akaunti zaidi ya 125,000 zilizokuwa zikisambaza habari za kichochezi zenye mlengo wa kundi hilo tangu katikati ya mwaka jana.

Wameleeza kuwa baada ya operesheni hiyo, mawasiliano ya kigaidi katika mtandao huo yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Kulikuwa na taarifa kuwa IS walikuwa wakitumia mtandao huo kuwashawishi vijana kujiunga nao na kwa kiasi fulani walifanikiwa.

KIKWETE: Tulikubali kurudiwa uchaguzi wa Zanzibar kwa shingo upande
Penzi la Nicki Minaj lamponza Meek Mill, Jaji amshushia nyundo ya kifungo