Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), mapema hii leo walifika makao makuu ya chama hicho wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuitaka Kamati Kuu kuwafukuza wanachama 19, wanaodaiwa kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho.

Tukio hilo lilitokea dakika chache kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA, ambayo ilipanga kukutana leo Ijumaa, Novemba 27 kuwajadili wanachama hao.

Wanachama hao 19 wakiongozwa na Halima Mdee waliapishwa na Spika wa Bunge Job Ndugai mapema juma hili, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, hali iliyozua taharuki kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA.

Hata hivyo mpaka sasa Kamati Kuu ya CHADEMa bado haijatoa majibu ya kikao kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, huku ikelezwa kuwa Halima Mdee na wenzake hawakuitikia wito.

Rage awaibia siri Simba SC
Uganda: Tume ya Uchaguzi yawaonya Polisi

Comments

comments