Takriban Wanajeshi wasiopungua 51 wameuawa baada ya kutokea kwa shambulio eneo la Sahel nchini Burkina Faso, katika mapigano makali yaliripotiwa kutokea kati ya wanajeshi wa Taifa hilo na kundi la kigaidi lenye silaha kati ya maeneo ya Oursi na Deou, katika jimbo la Oudalan.

Taarifa ya Jeshi hilo imesema, idadi hiyo ya vifo inaweza kuongezeka katika saa zijazo kwani wengi wa wanajeshi kadhaa bado hawajulikani walipo na karibu watu 80 bado wanatafutwa ikiwa ni saa chache kabla ya kutangazwa kwa vifo hivyo vya wanajeshi.

Mamlaka zinasema Wanajeshi waliojeruhiwa kwasasa wanatibiwa katika vituo vya matibabu na helikopta za jeshi la anga zimeanza kusafirisha miili ya wanajeshi waliouawa wakati wa shambulio hilo kwenda mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa majeshi, wanajeshi hao walikuwa katika majukumu yao ya kila siku na walishambuliwa na watu wenye silaha hali iliyosababisha mapigano makali kati ya maeneo ya Oursi na Deou, huko Sahel, karibu na mpaka wa nchi ya Mali.

Vifo juu ya vifo: Tetemeko jingine lauwa Uturuki, majeruhi 200
Dkt. Mpango aitaka Mahakama kuepusha malalamiko