Uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar umetangaza kuachana na wachezaji wanane, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ambao umepangwa kuanza mapema mwezi Oktoba.

Kagera Sugar inayonolewa na kocha kutoka nchini Kenya Francis Baraza imetangaza kuachana na wachezaji hao, na kuwatakia kila la la Kheri katika changamoto zao mpya kuanzia msimu ujao.

Uongozi wa klabu hiyo ya mkoani Kagera umetoa taarifa rasmi za kuachana na wachezaji hao na kuichapisha kwenye kurasa za mitandao za klabu hiyo.

Taarifa hiyo imeandikwa: ?????? ??? And GOODBYE

Uongozi wa Kagera Sugar Football Club unapenda kutoa taarifa kwa wanamichezo Pamoja na wanahabari kuwa, umeamua kutowaongeza mikataba mipya wachezaji 8 ambao mikataba yao imetamatika mwisho wa msimu wa 2020/2021 na kwa maamuzi hayo basi wachezaji hao wote hawatokuwa sehemu ya kikosi kiatakachoingia kambini katika maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara 2021/2022 ambayo inatarajia kuanza muda si mrefu.

Wachezaji hao ni Pamoja na: BENEDICT Tinocco (keeper), Haroun Mussa (Beki), Hassan Isihaka(Beki), Ali Sonso (Beki), Mohammed IBRAHIM  (Kiungo), Mussa Mossi (Kiungo), Abdulswamadu Kasim (Kiungo), Vitalis Mayanga (Mshambuliaji).

Makubaliano hayo yamefanyika baina ya Benchi la ufundi, wachezaji Pamoja na Uongozi na kufikia muafaka wa kuwaruhusu waende kutafuta changamoto sehemu nyingine ili waweze kuendeleza mapambano.

Uongozi unapenda kuwashukuru  kwa michango yao mikubwa walioionesha kuipambania timu  kwa kujitoa kwa hali na Mali tangu siku ya kwanza ambapo waliamua kuwa wanafamilia ya Kagera Sugar Hadi leo tunafikia tamati.

Mazuri yenu tutayaenzi na kuyakumbuka daima na hakika mmetuachia maswali magumu Sana Mioyoni mwetu lakini waswahili wanasema Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho.

Tunawatakia kila la Kheri katika changamoto zenu mpya mtakazoenda kukutana nazo katika tasnia hii ya mpira wa Miguu na Mungu awaongoze katika kila hatua mtakayokuwa mnaiendea katika mapambano mapya.

OBRIGADO A TODOS BROTHERS

Edo Kumwembe: Sioni haja ya Simba SC kufanya usajili
TBC kutangaza Ligi Kuu miaka kumi