Wafanyakazi wanawake, kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, wametoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaopatiwa matibabu ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – JKCI, ikiwa ni sehemu ya sherehe ya siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa WCF, Laura Kunenge amesema Wanawake hao pia wamegharimia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto watatu wenye uhitaji, waliolazwa kwenye Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Wanawake, tawi la Tughe, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Susan R. Reuben (kushoto) akimpa mkono mtoto Abdulrasul  Jumanne (12) anayesubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo, mara baaada ya WCF kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali na fedha za kugharimia upasuaji wa moyo kwa watoto watatu wenye uhitaji wanaopatiwa matibabu kwenye Taasisi ya JKCI.

Amesema, “ukimsaidia mama umesaidia familia nzima, tunaunga na wanawake wote Duniani katika kusherehekea siku ya wanawake Duniani na tunaungana na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha tunaisaidia jamii nzima, tunakuwa karibu na jamii yetu, kama ambavyo tunapenda familia zetu, familia ikiwa bora ni wazi maisha ya watanzania yanakuwa bora.” Alisema.

Aidha ameongeza kuwa, msada huo ni ishara kuwa WCF inaunga mkono juhudi zinazofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kitabibu na kwamba usaidizi wa mahitaji mbalimbali kutoka kwa jamii huongeza faraja kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu.

Msada uliotolewa na WCF ni sehemu ya sherehe za siku ya wanawake Duniani zinazofanyika Machi 8, kila mwaka.

Akiongea baada ya kupokea msada huo, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi JKCI, Robert Aloyce Malya amesema taasisi hiyo inapokea wagonjwa wenye uwezo tofauti tofauti, na kitendo cha Wanawake wa WCF kutoa msada huo ni faraja.

Baadhi ya Akina mama wanaouguza watoto wao JKCI wa matibabu ya moyo wamewashukuru wanawake toka WCF kwa msada huo ambao ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani inayofanyika Machi 8 kila mwaka.

Kesi ya uhaini: Kiongozi wa upinzani jela miaka 15
Ajali: Basi lauwa tisa Katavi, majeruhi wasimulia tukio