Serikali nchini, imesema Bima ya Afya kwa Wote ni suluhisho la kuondoa changamoto zilizopo kwa CHF, hivyo ni muhimu kila mwananchi kujiandaa kunufaika na vifurushi vitakavyopatikana kupitia bima hiyo pindi itakapoanza.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Dkt. Godwin Mollel katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri na taasisi za sekta ya Afya.

Naibu Waziri Wizara ya Afya, Dkt. Godwin Mollel.

Amesema, “Tulichowaambia Waganga wakuu kuwa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote utakuwa mwarobaini wa kuondoa matatizo ya ubovu uliopo ndani ya CHF ubora wa Huduma umeimarika kutoka asilimia 72% hadi asilimia 81% kupitia vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amekumbusha uongozi wa kuleta matokeo chanya katika utendaji huku akizungumzia umuhimu wa kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta ya Afya.

Sehemu ya washiriki katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na taasisi za sekta ya Afya.

Awali, Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania, Dkt.Best Magoma alisema mafanikio katika sekta ya afya ni pamoja na ujenzi wa Hospitali za Halmashauri ambapo serikali ilishatoa Tsh.Bilioni 123 .53 za ruzuku kuendeleza ujenzi wa hospitali 135 na kukarabati hospitali kongwe .

Naye Kaimu Mkurugenzi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga amesema Elimu ya Afya kwa Umma itaongeza nguvu kuelimisha Umma kuhusu masuala ya Afya, ikiwemo elimu Jumuishi.

Nabi: Bado kuna kazi kubwa Kimataifa
Sawadogo apata mtetezi Simba SC