Kiongozi wa Chama cha Upinzani wa Belarus, Sviatlana Tsikhanouskaya (40), anayeishi uhamishoni amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya jaribio la kutaka kufanya mapinduzi.

Tsikhanouskaya, ambaye aliwahi kuwa Mwalimu wa Kiingereza alikimbilia nchi jirani ya Lithuania mwaka 2020, baada ya kugombea uchaguzi wa rais dhidi ya kiongozi wa sasa Alexander Lukashenko aliyeshindwa kwa asilimia kubwa.

Makala: Mfahamu Rais mteule wa Nigeria, aliyekwepa kuingia jela akaingia Ikulu

Kiongozi wa Chama cha Upinzani wa Belarus, Sviatlana Tsikhanouskaya (40).

Akizungumzia hukumu hiyo amesema, ni adhabu ya kujaribu kukuza demokrasia ya Belarus na kusema hiyo haibadilishi uhalisia kuwa Lukashenko aliiba kura na kushinda isivyo halali katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Hata hivyo, madai hayo yamekuwa yakikanushwa vikali na Lukashenko ambaye ni rafiki wa karibu wa rais wa Russia Vladimir Putin, ametawala Belarus kimabavu kwa karibu miongo mitatu hali iliyopelekea maandamano makubwa ya kitaifa dhidi ya utawala wake.

Siku ya Wanawake Duniani: REA yatoa Majiko Banifu 114
Wanawake WCF wagharamia matibabu upasuaji wa moyo