Watu mbalimbali maarufu wameoneshwa kushtushwa na kusikitishwa na kifo cha  aliyekuwa mchekeshaji majukwaani na mtandaoni Martha Micheal maarufu kama  ‘Bossmartha’ aliyefariki dunia jana alfajiri katika hospitali ya Kisarawe alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.

Mmoja wa kiongozi wa kundi hilo Coy Mzungu amesema kuwa ” licha ya Martha kuwa mzazi mwenzake na msanii wa WCB Mbosso pia ameacha pengo kubwa kwenye Tasnia ya uchekeshaji jukwaani (stand up comedy) kutokana na uwezo wake wa kuchekesha watu kwamambo ya uswahilini.

”Martha alikuwa ni miongoni mwa wachekeshaji wanaofanya vizuri katika tasnia hii kwa upande wa wanawake kifo chake kitabaki kuwa kovu katika tasnia na kikundi, taratibu za mazishi zinafanyika yumbani kwao Tabata kimanga ambapo msiba upo” alisema Coy Mzungu

Aidha baadhi ya mastaa akiwemo Wolper, Nandy , Beka flevour, na wengine wengi wametuma salamu zao za pole kupitia mitanda ya kijamii kwa ndugu na marafiki wa marehemu Martha,

Aidha marehemu  Martha alishawahi kushiriki kwenye baadhi ya kazi za wasanii wa bongo fleva alishiriki kwenye  kwenye video ya Whozu ‘Roboti’ ilyotoka mwaka huu.

 

Ilibaki kidogo Pogba aondoke Old Trafford
TFF yashtakiwa FIFA.