Takriban watu 12 wamefariki dunia na wengine wapato 13 kujeruhiwa mapema leo kufuatia mkanyagano katika jumba la kidini la Mata Vaishno Devi huko Kashmir India.

Jumba hilo ambalo hutembelewa na maelfu kila siku kwa ajili ya maombi limeleta maafa baada ya watu wengi kufika kutoa heshima zao kuelekea mwaka mpya wa 2022.

Taarifa kutoka vyombo vingi vya habari zinasema kuwa zaidi ya watu 20 wamepata majeraha zaidi ikiwa picha mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa magari ya wagonjwa yakikimbilia eneo la tukio.

Kupitia kurasa mbalimbali za kijamii Rais wa India Rashtrapati Bhavan, ametoa salam zake za pole na kusema ameshtushwa na tukio hilo ambapo ni eneo watu walilokwenda kwa ajili ya ibada huku akiwatakia uponyaji wa haraka wote waliopata majeraha.

Jumba hilo la kidini la Mata Vaishno Devi ni maarufu kwa dhehebu la Hindu

Makamu wa Rais ashiriki Misa ya Mwaka mpya
Mapenzi ya jinsia moja Kenya Kizungumkuti