Watu 9 kisiwani Zanzibar wamewekwa ndani pamoja na Bar tatu kufungwa kwa makosa mawilli tofauti tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Ambapo watu hao 9 wamekamatwa kwa kula chakula mchana katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Bar tatu nazo zimefungwa kutokana na kuuza chakula mchana katika mkoa wa mji wa Magharib Unguja hadi kumalizika kwa mwezi Ramadhani.
Mkuu wa Mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud ameziagiza Manispaa zote kusitisha leseni ya biashara za vileo katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema hatua hiyo itaimarisha imani za watu na kuzitaka Manispaa hizo kusimamia agizo hilo na kufuata kanuni za Wizara ya Afya ili kuepusha mripuko wa maradhi.
”Ili waumini waweze kuukabili mwezi huu lazima kwa wanachi kutumia fursa za Ramadhani kwa kufanya mambo mema ili Allah azikubali swaumu zetu” Amesema Ayoub.
Mbali na hilo amewataka wafanya biashara wa bidhaa za chakula na nafaka kupunguza bei za bidhaa ili wananchi wanyonge waweze kumudu na kununua bidhaa hizo kwa ajili ya futari kwani Serikali ya Zanzibar imetoa punguzo la kodi kwa bidhaa za nafaka na chakula zinazotoka nje ya Zanzibar.