Serikali inapanga kuwajengea watumishi wa Hospital ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara, nyumba 20 na kununua magari mawili aina ya Coaster na gari kwa ajili ya Mkurugenzi ili kuwasaidia kutekeleza majukumu yao vizuri.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa ziara katika Hospiyali hiyo kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa vyumba mbalimbali vya kutolea huduma ya Afya kwa wagonjwa.

“Nimefurahi sana kuona hospitali hii imefika katika hatua hii baada ya kutelekezwa takribani miaka 30, namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutugawia fedha takriban zaidi ya Bil. 10 kwa kutekeleza ahadi yake ya kuendeleza miradi yote iliyoanza miaka mitano iliyopita,” amesema Waziri Ummy.

Aidha, amesema awamu ya tano iliwekeza kwenye majengo na sasa awamu ya sita inawekeza kwenye vifaa ambavyo vimepatikana katika hospitali hiyo ni pamoja na MRI, CT-Scan, ufungwaji wa Digital Xray mashine mbili, Mobile digital X-ray mbili, Ultra-Sound mbili na vifaa vingine.

Waziri Ummy amewataka wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanawalipa stahili zao watumishi wote wapya wa Afya kwa wakati ili waweze kurudi haraka kwa kuwa kuna wengine hawajaingizwa kwenye mfumo wa malipo (Payroll).

“Naomba watumishi wote nchini ambao mmeenda kuripoti katika vituo vyenu vipya vya kazi baada ya siku 14 mrudi katika maeneo yenu ya kazi, na Tunafurahi kwakuwa wengi mmeripoti,” amesema Waziri Ummy.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy aliambatana na viongozi wengine kutoka wizara ya Afya pamoja na viongozi kutoka katika Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo Brig. Gen. Marco Gaguti

Urusi yatafuta ushirika Afrika
Yondani aahidi mazito Kombe la Shirikisho Afrika